1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM. Viongozi wa ngazi za juu wafanya mazungumzo na rais El Bashir wa Sudan

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6r

Viongozi wa ngazi za juu wamefanya mazungumzo na rais Omar el Bashir wa Sudan kwa lengo la kumshawishi rais huyo juu ya ulazima wa kutatua mgogoro wa jimbo la Darfur na akubali kupelekwa askari wa umoja wa mataifa ili kulinda amani katika jimbo hilo.

Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya bwama Emanuel Barosso ameeleza wasiwasi mkubwa juu ya hali ya Darfur na amesema kuwa anafanya juhudi ili suluhisho lifikiwe kwa njia ya mazungumzo

Otton………….Inatubidi tuseme kwa uwazi kabisa kwamba hali haiwezi kuendelea kama ilivyo sasa na wala haikubaliki. Ni lazima tuibadili kwa misingi ya makubaliano ya amani ya Darfur. Lengo letu ni amani hakuna ajenda nyingine.

Baraza la usalama a la umoja wa mataifa hivi karibuni lilipitisha azimizo juu ya kupelekwa wanajeshi alfu 20 wa umoja wa mataifa katika jimbo la Darfur.