1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Mwito wa kutotumia nguvu Ukraine

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBy8

Viongozi wa Ukraine kujadili njia ya kutenzua mgogoro wa kisiasa nchini humo.Ujerumani imeungana na Urusi kutahadharisha viongozi wa Ukraine kutotumia nguvu kuutenzua mzozo huo.Afisa wa kibalozi wa Ujerumani,Johannes Regenbrecht alisema kwenye mkutano na Waziri Mkuu wa Ukraine,Viktor Yanukovich kuwa kila njia yapaswa kutumiwa ili kuzuia ghasia katika kinyanganyiro cha madaraka kati ya Waziri Mkuu Yanukovich na Rais Viktor Yushchenko,kwani hali hiyo itaathiri uhusiano kati ya Ukraine na Ulaya. Mvutano kati ya viongozi hao wawili,ulifikia upeo mpya siku ya Ijumaa,rais Yushchenko alipoamua kuvidhibiti vikosi vya usalama wa ndani,ambavyo kwa kawaida husimamiwa na waziri wa mambo ya ndani.