1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Wanadiplomasia wa Ufaransa wafunga virago

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpQ
Kizza Besigye wa chama cha upinzani Uganda
Kizza Besigye wa chama cha upinzani UgandaPicha: dpa

Wanadiplomasia wa Ufaransa na familia zao leo wamekuwa wakifungasha kwa haraka na kujiandaa kuondoka Rwanda baada ya serikali kuvunja uhusiano wake na nchi hiyo katika mzozo mkubwa wa kidiplomasia.

Wakikabiliwa na agizo linalowataka wawe wameondoka nchini humo kufikia Jumatatu wafanyakazi wa ubalozi wa Ufaransa mjini Kigali kadhalika waajiriwa wa taasisi nyegine zote za serikali ya Ufaransa zilizoagizwa kufungwa wako tayari kuondoka.

Balozi wa Ufaransa anatarajiwa kuondoka Kigali jioni hii.

Rwanda ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na kitamaduni na Ufaransa hapo jana baada ya hakimu wa Ufaransa kumhusisha Rais Paul Kagame na wasaidizi waandamizi katika mauaji ya mwaka 1994 ya aliekuwa kiongozi wa nchi hiyo Juvenal Habyariman ambayo yamechochea mauaji ya kimbari nchini humo.