1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Mgombea Urais wa zamani ashtakiwa kwa uhaini

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCh6

Mgombea wa Urais wa zamani amesimama kizimbani kujibu mashtaka ya uhaini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hapo jana siku moja baada ya mahkama kutupilia mbali madai ya upinzani kwamba inatengwa kusiko haki bungeni.

Marie-Therese Nlandu na washtakiwa wenzake tisa wamefikishwa mbele ya mahkama ya kijeshi katika mji mkuu wa Kinshasa wakishtakiwa kwa shambulio la kuteketeza kwa moto Mahkama Kuu tendo lilofanywa na kundi la upinzani mwezi uliopita.

Wakati wa shambulio hilo la Novemba 21 mahkama ilikuwa inasikiliza rufaa ya kiongozi wa upinzani Jean-Piere Bemba dhidi ya ushindi wa Urais wa Joseph Kabila katika marudio ya uchaguzi ya mwezi wa Oktoba.Rufaa hiyo ilikataliwa siki sita baadae.

Nlandu alikuwa mgombea wa Urais wa kujitegemea hapo mwezi wa Julai lakini baadae alimuunga mkono Bemba na iwapo atapatikana na hatia anaweza kukabiliwa na adhabu ya kifo kutokana na mashtaka kuanzia uasi hadi kumiliki silaha kinyume na sheria.

Washtakiwa wengine wanaweza pia kukabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka 20 gerezani.