1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa.Vikosi vya Ulinzi vya Umoja wa Mataifa vyaongeza ulinzi mjini Kinshasa.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1J

Vikosi vya kijeshi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa vilivyoko nchini Kongo, vimeanza kufuatilia kwa karibu harakati za kijeshi mjini Kinshasa, ikiwa inakaribia wakati wa marejeo ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi huu.

Harakati hizo zimekuja kufuatia taarifa za kutokea mapigano katika mikoa kadhaa baina ya wafuasi wa Rais Joseph Kabila na mpinzani wake makamo wa Rais Jean-Pierre Bemba.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamewekwa tayari karibu na vituo vitano ili kukagua nyendo zozote za watu na wanajeshi pembezoni mwa mto katika mji mkuu ambao ulikubwa na mapigano mwezi August kati ya wanajeshi wanaowatii wagombea urais wa nchi hiyo.

Tahadhari zaidi imeongezeka katika kipindi hiki cha kura ya marejeo ambayo inatazamiwa kufanyika tarehe 29 mwezi huu.