1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea mbili zashindwa kutatua mgogoro wa mpakani

14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cbgn

Mazungumzo ya kijeshi ya ngazi za juu, kati ya Korea ya kaskazini na kusini yamemalizika bila ya kukubaliana kuhusu eneo lililopendekezwa la kuvulia samaki.Ujumbe wa ngazi za juu kutoka pande zote mbili, ulikuwa unakutana katika kijiji cha mpakani cha Panmunjon. Pande zote zimeshindwa kutuoa ufumbuzi wa mpaka wake katika bahari.Korea hizo mbili zilikuwa zinajaribu kuumaliza mvutano uliopo katika mpaka wake katika bahari ya njano tangu mkutano wa Oktoba kwa nia ya kuepusha mvutano kama ule uliotokea mara mbili, mwaka wa 1999 na 2000.Meli za kijeshinza nchi hizo mbili zilitupiana makombora mara hizo mbili.