1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS:Wafanyikazi wawili wa kiwanda cha Uchina waokolewa

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBut

Jeshi nchini Nigeria limevamia maficho ya genge moja la wapiganaji na kuwaokoa wafanyikazi wawili wa kiwanda cha mafuta walio na asili ya Uchina.Wafanyikazi hao walitekwa na kundi moja zaidi ya miezi miwili iliyopita katika eneo la kusini magharibi.

Kwa mujibu wa magazeti katika eneo hilo maafisa wa kijeshi walivamia maficho hayo katika jimbo la Ebonyi baada ya kudokezwa taarifa hizo.Kulingana na gazeti la Vanguard mfanyikazi wa pili aliyetekwa Machi 17 kutoka kiwanda kinachoendeshwa na Wachina mjini Nnewi bado hajulikani aliko.

Majina ya watu hao wawili hayajatajwa hadharani nao wanadiplomasia wa Uchina hawataki kuzungumzia suala hilo.Hii ni mara ya kwanza wafanyikazi wa kigeni wametekwa katika jimbo la Anambra.Mateka wengi hukamatwa katika eneo la kusini lililo na mafuta mengi.Takriban wafanyikazi 190 wa kigeni wametekwa katika eneo hilo na kuachiwa baada ya majuma au siku chache.