1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lebanon bado haina rais

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaBM

BEIRUT.Spika wa Bunge nchini Lebanon ametangaza kusogeza mbele uchaguzi wa rais nchini humo hadi Jumatatu ijayo.

Hii ni mara ya nane kwa bunge kuahirisha kufanya uchaguzi huo, kutokana na mvutano uliyopo kati ya kambi mbili hasimu ile inayounga mkono serikali na ile inayoungwa mkono na Syria.

Mara ya mwisho uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na kupingwa kwa utaratibu wa kuifanyia mabadiliko katiba ya nchi hiyo, kitu ambacho kinatakiwa kufanyika kabla ya mgombea aliyeteuliwa Mkuu wa Jeshi General Michel Suleiman kuweza kuchaguliwa.

Lebanon imekuwa haina Rais toka kumalizika kwa kipindi cha kuwa madarakani Rais wa zamani Emile Lahoud mwezi uliyopita.