1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON:Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakubaliana kufanya mageuzi ya katiba

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EV

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameidhinisha mageuzi ya makubaliano ya Umoja huo kuhusu katiba.Makubaliano hayo mapya yanaanza kutimizwa mwaka 2009 endapo kura za maoni aidha mabunge husika yatapitisha azimio hilo.Mkwamo huo wa katiba ulitokea baada ya Uholani na Ufaransa kukataa rasimu ya katiba mwaka 2005. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya Jose Socrates ambaye ni Waziri Mkuu wa Ureno,makubaliano hayo yatatiwa saini mjini Lisbon ifikapo Disemba 13.

''Safari hii hakukuwa na visababu na sababu za kuwafanya viongozi wa mataifa na serikali kutoafikiana.Ni mafanikio makubwa.Tunaweza katika dakika ya mwisho kutafuta suluhu ya baadhi ya mambo ambayo bado yanatatiza tukiwa na mtizamo wa pamoja wa Ulaya''

Azimio hilo linalenga kufanya mageuzi katika katiba ya uMoja wa Ulaya tangu mataifa 10 ya kikomunisti ya zamani pamoja na Bulgaria na Romania kujiung na muungano huo mwezi Januari mwaka huu.Viongozi wa Umoja wa Ulaya waliafikiana baada ya majadiliano ya siku mbili kuhusu nchi za Poland na Italia zilizopinga baadhi ya vipengee.

Makubaliano hayo yanajumuisha mipango ya kubadili sera za kigeni za Umoja huo pamoja na uteuzi wa rais wa kudumu muda mrefu zaidi badala ya uongozi wa kupokezana kila miezi sita.