1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Blair ataka vikwazo zaidi kwa utawala wa Mugabe.

22 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGf

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kuwa atashinikiza kwa umoja wa Ulaya kupanua uwigo wa vikwazo dhidi ya utawala wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Blair ameliambia bunge kuwa pia atalitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kukemea dhidi ya hali nchini humo, ambayo ameiita , kuwa ni mbaya na ya kusikitisha, ambayo ni maafa kwa watu wa Zimbabwe.

Blair pia amesisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika kuweka mbinyo dhidi ya Mugabe.

Morgan Tsvangirai, kiongozi wa chama cha upinzani cha Movemenz for Democratic Change, ni mmoja miongoni mwa watu kadha wanaharakati ambao walijeruhiwa vibaya katika hatua za hivi karibuni za serikali kuzima mkutano wa chama hicho.