1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Gordon Brown athibitishwa kuwa ndie kinara wa Labour

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoV

Gordon Brown amethibitishwa kuwa kinara wa chama cha Labour nchini Uingereza siku chache zikiwa zimesalia kabla ya kuchukua wadhfa wa uwaziri mkuu wa nchi hiyo.

Katika dhifa maalum iliyofanyika mjini Manchester bwana Browm aliwaambia wanachama wa Labour kuwa lazima chama hicho kibadilike na kwamba amejifunza mengi kutokana na maamuzi ya waziri mkuu anaeondoka Tony Blair kuhusu vita vya Irak.

Matokeo ya kura ya maoni yanaonyesha kuwa chama cha Labour kimeongeza umaarufu wake kutokana na kuchaguliwa kwa bwana Gordon Brown kukiongoza chama hicho ambacho kilipoteza umaartufu wake kwa sababu ya vita vya Irak.