1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mgogoro wa Darfur usipewe kisogo

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPF

Wanaharakati katika nchi 30 mbali mbali hii leo wanafanya maandamano kuwahimiza viongozi wa kimataifa wanaokusanyika kwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,kutoupa kisogo mgogoro wa Darfur.

Colleen Connors wa “Globe for Darfur“-muungano wa makundi ya misaada yanayofanya kazi Darfur amesema,viongozi wa kimataifa wamekubali,kuna matumizi ya nguvu katika Darfur na wameahidi kukomesha ukatili huo.Sasa wanapaswa kutimiza ahadi hiyo.