1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mwanamfalme wa Uingereza, Philip afanya ziara nchini Irak

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzz

Mwanamfalme wa Uingereza Philip, mumewe Markia Elizabeth wa II, alifanya ziara isiotarajiwa nchini Irak na kuwatembelea wanajeshi wa Uingereza katika mji wa Basra kusini mwa nchi. Makao ya Markia ya Uingereza Buckingham Palace, yamesema mwanamfalme Philip, mwenye umri wa miaka 85 sasa, amewatembelea wanajeshi wa Uingereza wanaomaliza muda wao wa miezi 6 kwenye meli ya Queen’s Royal ambayo ilikuwa ikishika doria kwenye eneo la mpaka kati ya Irak na Iran.

Mwanamfalme Philip ambae ndie kamanda wa heshima wa kikosi hicho cha wanamaji, aliwaambia wanajeshi wa Uingereza kwamba wamefanya kazi kubwa na yenye kupendeza. Alisema raia wa Uingereza wanatambua juhudi wanazozifanya kusaidia kuboresha hali ya mambo nchini Irak.