LONDON, Uingereza yafikiria kuwatimua wanadiplomasia wa Urussi
12 Julai 2007Matangazo
Uingereza inafikiria kuwafurusha wanadiplomasia wa Urussi nchini humo kufuatia nchi hiyo kukataa kumkabidhi mtu anayetuhumiwa kwa mauaji ya mkosoaji mkubwa wa Urussi Alexander Litvinenko mwaka jana.
Taarifa hizo zimechapishwa na magazeti mbali mbali ya Uingereza hii leo.Uhusiano kati ya Uingereza na Urussi umekuwa wa mivutano katika miezi ya hivi karibuni hasa baada ya Urussi kudinda kumkabidhi Andrei Lugovoi kwa Uingereza ili kukabiliwa na mashtaka ya mauaji ikidai sheria yake hairuhusu jambo hilo kufanyika dhidi ya raia wake.