1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Wanajeshi wa Uingereza wawasili.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCM

Wanajeshi wanamaji na wanajeshi wa kawaida 15 wa Uingereza ambao walikuwa wanashikiliwa na Iran kwa muda zaidi ya siku 13 zilizopita wanaelekea mjini London kutoka uwanja wa ndege wa Tehran.

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad ameuambia mkutano wa waandishi wa habari uliotangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari duniani , kuwa ameamua kuwapa msamaha wanajeshi hao katika kile alichokieleza kuwa ni zawadi kwa watu wa Uingereza.

Akizungumzia kuachiwa kwa wanajeshi hao waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kuwa kuachiwa kwao kumekuwa ni faraja kubwa sio kwao tu bali hata kwa familia zao.

Televisheni ya Iran baadaye ilionyesha picha za rais Ahmedinejad akizungumza na wanamaji hao. Wanajeshi hao wa Uingereza walikamatwa March 23 katika eneo la maji la Shatt al-Arab kati ya Iraq na Iran. Iran inasisitiza kuwa wanajeshi hao walikuwa katika eneo la maji la Iran , dai ambalo Uingereza inalipinga vikali.