1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Washukiwa wa ugaidi wakamatwa Uingereza

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3f

Watu wanne, akiwemo mjane wa mtu aliyeongoza mashambulio ya bomu ya Julai mwaka 2005, wamekamatwa kuhusiana na mashambulio hayo nchini Uingereza.

Watu hao wanne wanashukiwa kwa mipango ya kutekeleza, kuandaa na kuchochea vitendo vya kigaidi.

Polisi wamewakamata watu hao baada ya msako katika maeneo ya West Yorkshire na Midlands.

Washukiwa hao waliohojiwa na wachunguzi wa shirika la upelelezi la Scotland Yard kuhusiana na mashambulio ya bomu ya Julai Saba, mwaka 2005 dhidi ya vyombo vya usafiri mjini London.

Kiasi watu hamsini na wawili walifariki na wengine mia saba wakajeruhiwa kwenye tukio hilo.