1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Bhutto asema Musharraf akubali kujiuzulu wadhifa wa mkuu wa jeshi

29 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUu

Rais wa Pakistan Pervez Musharraf amekubali kujiuzulu kama amiri jeshi mkuu katika ule mpango wa kugawana madaraka na aliyekuwa waziri mkuu wa nchini Benazir Bhutto.

Hayo yamedokezwa na kiongozi huyo wa zamani aliyeko uhamishoni nchini Uingereza Benazir Bhutto katika mahojiano yake na gazeti moja la Uingereza yaliyochapishwa hii leo.

Matamshi ya Bhutto yamekuja siku moja baada ya waziri na mbunge wa chama tawala kujiuzulu kupinga mpango wa rais Musharraf wa kutaka kuchaguliwa tena kama rais akiwa bado mkuu wa majeshi.Wapinzani wa rais Musharraf wanasema kuchaguliwa tena kuwa rais akiwa mkuu wa majeshi ni kitu kisichokubalika na kukiuka katiba.

Wakati huo huo waziri mkuu mwingine wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif amesema atarudi nchini mwake katika muda wa wiki mbili kuanzia leo kuongoza kampeini ya kumuondoa madarakani rais Musharaf.