1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Brown awa waziri mkuu mpya wa Uingereza

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnl

Gordon Brown leo hii amekuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya kung´atuka kwa Tonny Blair.

Gordon Brown mwenye umri wa 56 ambaye alikuwa waziri wa fedha katika serikali ya Blair kwa muda wa miaka kumi, anatarajiwa kutangaza baraza lake jipya la mawaziri.

Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 17 kwa Uingereza kupata Waziri Mkuu mpya bila ya uchaguzi

Kwa upande wake, Tonny Blair, alimaliza rasmi kazi zake kama waziri mkuu hii leo kwa kuhudhuria kipindi cha maswali na majibu katika bunge la mabwanyenye.

Akijibu swali jinsi ya kupatikana kwa amani katika mashariki ya kati, Blair alisema kuwa sulihisho kati ya Israel na Palestina ni muhimu kufikia lengo hilo.

Inaelezwa kuwa Blair anatarajiwa kutangazwa kuwa mjumbe maalum wa pande nne zinazotafuta amani ya mashariki ya kati.