1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London.Madona atua Uingereza na mtoto wake wa kupanga.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD22

Mwanamuziki maarufu Madonna na mtoto wa kiume Mmalawi mwenye umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja anayepanga kumchukua kama mtoto wa kupanga wamewasili nchini Uingereza.

Kundi la kutetea haki za binadamu nchini malawi linapanga kupambana kisheria kuzuwia hatua hiyo likisema kuwa inakwenda kinyume na utaratibu wa kawaida.

Chini ya sheria za Malawi , watu kutoka nje ni lazima waishi katika nchi hiyo kwa muda wa miezi 18 kabla ya kuweza kupata haki kamili za kupanga watoto.

Madonna alipewa haki ya muda na mahakama ya malawi Alhamis wiki iliyopita inayomruhusu kupanga mtoto huyo wa mkulima.

Amekuwa nchini humo kwa muda wa wiki moja akitathmini mradi wa kuwasaidia watu wenye ukimwi ambao anaufadhili.

Anatakiwa kurejea Malawi ili kukamisha hatua hizo za upangaji.