1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON.Uingereza kudhibiti wimbi la wahamiaji kutoka Romania na Bulgaria

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzb

Romania na Bulgaria zimekasirishwa na tangazo la Uingereza juu ya kuweka uthibiti katika uhuru wa ajira kwa wahamiaji kutoka nchi hizo baada ya nchi hizo kujiunga na umoja wa ulaya mwaka ujao.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza John Reid hata hivyo amesema kuwa sekta ya kilimo na viwanda vya chakula itakuwa wazi kwa wananchi wa nchi hizo mbili ambao hawana ujuzi wa kazi zingine.

Uingereza, Ireland na Sweden ndio nchi pekee zilizoweka wazi soko la ajira kwa wahamiaji kutoka nchi nane za ulaya mashariki tangu nchi hizo zilipo jiunga na umoja wa ulaya mwaka 2004.

Kutoka wakati huo zaidi ya wahamiaji laki tano kutoka nchi hizo wengi wao kutoka Poland wamehamia nchini Uingereza.

Utawala nchini Uingereza ulikisia takriban wahamiaji 15,000 tu wangeingia nchini humo kwa mwaka.