1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUANDA: Ndege ya shirika la TAAG yapata ajali

29 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnW

Ndege ya Angola ikiwa na abiria 78 imepata ajali.Shirika la habari la Angola limeripoti kuwa ndege aina ya Boeing 737 ya shirika la TAAG, iliondoka mji mkuu Luanda na ilijaribu kutua Mbanza Congo.Watu wasiopungua 6 wamepoteza maisha yao.Ajali hiyo imetokea siku ambayo Kamisheni ya Ulaya imetangaza mipango ya kuorodhesha upya mashirika ya ndege yanayosemekana kuwa si salama. Orodha hiyo imelitaja shirika la ndege la Angola,TAAG na mashirika yote ya ndege ya Indonesia yapatao 51 ikiwa ni pamoja na Garuda.Vile vile mashirika mengi ya ndege kutoka Urusi na Ukraine yametajwa katika orodha mpya.