1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Mashabiki wa mpira 12 wapoteza maisha

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvM

Mashabiki wa mpira 12 wamefariki na kama 46 wengine walijeruhiwa katika mkurupuko uliotokea kwenye uwanja wa michezo,kaskazini mwa Zambia. Mkurupuko huo wa watu ulitokea baada ya kumalizika mchezo wa mpira kwenye uwanja wa Chililabombwe,ulio karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Katika mchezo huo wa kugombea nafasi ya kuingia katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Kiafrika,Zambia iliikandika Congo mabao 3-0.