1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yaendelea kwa usiku wa pili nchini Ufaransa

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTXg

Kwa usiku wa pili mfululizo, polisi wa Ufaransa wamefyatua gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira wakati walipokabiliana na waandamanaji kaskazini mwa mji mkuu Paris.

Vijana waliojawa na hasira wamewashambulia maafisa wa polisi kwa mawe na kuchoma motokaa na majumba kwa usiku wa pili kwenye kitongoji cha Villiers- le- Bel.

Zaidi ya maafisa 30 wakiwemo pia wazima moto wamejeruhiwa wakati wa machafuko hayo ya usiku wa kuamkia leo.

Chanzo cha machafuko hayo ni vifo vya vijana wawili katika ajali iliyoihusisha motokaa ya polisi.

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, akiwa ziarani nchini China, na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wakati wa machafuko ya mwaka wa 2005, ametoa mwito kuwe na utulivu.

Ametaka vyombo vya sheria vipewe nafasi vichunguze ni nani aliyesababisha vifo vya vijana hao.