1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahabusi wawili wa Colombia waachiwa huru na wanamgambo wa FARC

Hamidou, Oumilkher11 Januari 2008

Rais wa Venezuela Hugon Chavez afanikiwa katika juhudi zake za kuwashawishi wanamgambo wa FARC wawaachie huru mahabusi.

https://p.dw.com/p/Co9U
Consuelo Gonzales na Clara RojasPicha: AP/DW


Mahabusi wawili waliokua wakishikiliwa kwa zaidi ya miaka sita na wapiganaji wa chini kwa chini wa FARC katika misitu ya Colombia wameachiwa huru jana na kupelekwa Caracas walikokutana na familia zao.Rais Alvaro Uribe wa Colombia amekiri juhudi za rais wa venezuela Hugo Chaves zimeleta tija.



Wanawake wawili,raia wa Colombia,Clara Rojas na Consuelo Gonzales wameachiwa huru katika opereshini ya kusisimua ya msituni iliyoandaliwa na Colombia na Venezuela kwa ushirikiano pamoja na kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu.Helikopta ndio iliyowasafirisha hadi katika ardhi ya Venezuela walikosafirishwa kwa ndege ndogo chapa ya Falcone hadi Caracas walikolahikiwa na familia zao pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Venezuela.


"Ni sawa na kuzaliwa upya.Nnahisi kama ni ndoto"amesema mbunge wa zamani wa Colombia Consuelo Gonzales mwenye umri wa miaka 57,aliyetekwa nyara september 10 mwaka 2001,huku machozi yakimtoka alipowaona binti zake na mjuukuu wake wa miaka miwili.


Clara Rojas,wakili mwenye umri wa miaka 44,amekumbatiana na mamaake mwenye umri wa miaka 76.

Familia ya Consuelo Gonzales walivaa fulana zilizoiandikwa "Wote wafuinguliwe hivi sasa."


Clara Rojas ni mshirika mkubwa wa mgombea wa zamani wa kiti cha rais nchini Colombia,raia wa Ufaransa na Colombia Ingrid Betancourt,waliotekwa nyara pamoja february 23 mwaka 2002.


Katika mahojiano pamoja na Radio ya Colombia,bibi Gonzales amezungumzia hali ngumu wanayokabiliana nayo mahabusi wakiume wanaoshikiliwa na wanamgambo wa FARC wanaofuata nadharia ya Marx.Mbunge huyo wa zamani wa Colombia anasema mahabusi hao wanafungwa pingu miguuni usiku na mchana.


Kwa upande wake rais Alvaro Uribe wa Colombia amekiri juhudi za upatanishi za kiongozi mwenzake wa Venezuela ndizo sababu ya kuachiliwa huru mahabusi hao.Rais Ulribe amewasihi wanamgambo wa FARC wakubali kushiriki katika mazungumzo ya amani yatakayokua kama anavyosema "ya dhati,na ya kidemokrasi."



Alikua rais Hugo Chavez aliyetangaza hapo awali kuachiliwa huru mahabusi hao,baada ya juhudi zake kushindwa december iliyopita.


"Wako huru na nnawatakia maisha mema" amesema rais Chavez mbele ya waandishi habari mjini Caracas.

Rais Chavez amewapongeza pia wanamgambo wa FARC kwa uamuzi wao.

Wanamgambo wa Farc wanasema wako tayari kuwaachia huru mahabusi wengine 43 ,ikiwa ni pamoja na Ingrid Betancourt na wamarekani watatu ikiwa wanaharakati wao 500 wataachiwa huru.Itafaa kusema hapa kwamba wanamgambo wa FARC wanawashikilia zaidi ya mahabusi 750.








►◄