1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yashindwa kumshtaki waziri mkuu Lesotho

Ibrahim Swaibu
24 Februari 2020

Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane amefika mahakamni Juma tatu, lakini hakushtakiwa na kosa lolote la uhalifu.

https://p.dw.com/p/3YL7D
Thomas Thabane 16.08.2014
Picha: Imago/Xinhua

Waziri mkuu wa LesothoThomas Thabane amefika mahakamni Juma tatu, lakini hakushtakiwa na kosa lolote la uhalifu. Mke wake wa sasa Maesaiah ambaye yuko kwenye dhamana naye akikabiliwa na kesi hiyo, alimsindikiza Thabane hadi mahakamani.

Hii imekuwa mara yake ya kwanza kuonekana hadharani tangu kushindwa kufika mahakamani Ijuma wiki iliyopita, hatua ambayo imewashangaza raia wengi nchini humo.

Thabane anashtakiwa na polisi kwa mauaji ya aliyekuwa mke wake, Lipolelo Thabane. Wakili wake waziri Qhalehang Letsika amesema kwamba waziri mkuu huyo amefika mahakamani  ili kuthibitisha kuwa alikuwa hakaidi amri ya mahakama.

Waziri mkuu Thabane alitaraijiwa kukabiliwa na kesi ikiwemo mauaji, jaribio la  kuua na pia ubadhirifu mkubwa wa mali, kufuatia kuauwa kwa Lipolelo kwa kupigwa risasi mnamo mwaka 2017.

Lesotho Maseru | First Lady Maesaiah Thabane
Maesaiah mke wa sasa wa waziri Thabane pia anakabiliwa na kesi hiyoPicha: DW/A. Kriesch

Mnamo wiki jana, Ijuma, naibu kamishna wa polisi nchini Lesotho Paseka Mokete alithibitisha kuwa waziri mkuu huyo atakabiliwa na kesi tatu ikiwemo ile ya mauaji ya mke wake wa kwanza. Lakini mwendesha mashtaka mkuu Hlalefang Motinyane  ameeleza kuwa bado kungali na masuala mengi ya kujadili na polisi kabla kuendelea na mashtaka.

Aidha jaji wa mahakama hiyo ametaka mahakama ya kikatiba ifafanue iwapo waziri mkuu alieko madarakani anaweza kukabiliwa na mashtaka yoyote ya uhalifu wakati bado angali mamlakani. Haijafahamika ni lini mahakama ya kikatiba itasikiliza kesi hiyo.

Wiki iliyopita,Thabane aliondoka hadi Afrika Kusini kwa kile msaidizi wake alichosema kuwa alienda kupokea matibabu na kushindwa kuonekana mahakamani.

Soma zaidi Waziri mkuu wa Lesotho ameshindwa kufika mahakamani

Thabane ambaye amekabiliwa na shinikizo kubwa kutoka chama chake cha ''All Basotho Convention'' (ABC) la kumtaka ajiuzulu kutokana na  kashfa hiyo, alitanganza kuwa atastafu Julai mwaka huu.

Mapema Juma tatu, msemaji wa chama hicho Montoeli Masoetsa alisema kuwa wanataka waziri mkuu ajiuzulu mara moja akiongeza kuwa nafasi yake iko tayari kuchukuliwa na mwenyekiti wa ABC Samuel Rapapa.

Vyanzo:DPAE/APE