1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maharamia wa kisomali

12 Aprili 2009

Majadiliano na wazee wa kisomali yavunjika

https://p.dw.com/p/HVFD
Marekebu na maharamiaPicha: AP

Majadiliano ya kumkomboa nahodha wa meli ya kimarekani alietekwa nyara katika bahari ya Hindi na maharamia wa kisomali yanaripotiwa yamevunjika. Maharamia wa kisomali waliomtia nguvuni nahodha Richard Phillips, wameonya kuwa kutumia nguvu kumkomboa nahodha huyo kutamalizikia kwenye msiba.

Gazeti la NY Times , limeripoti kuwa majadiliano na kikundi cha wazee wanaowaakilisha maharamia hao yamekwama-masaa tu baada ya maharamia hao walipokifyatulia risasi chombo kidogo cha kikosi cha wanamaji cha Marekani kilichojaribu kuikaribia marekebu ya uokozi anamoshikiliwa nahodha Phillips.

Kikosi cha wanamaji cha Marekani,kina manuwari 2 katika eneo hilo huku kisa hiki kikiingia siku yake ya 4 tangu kuanza.Meli ya nahodha Phillips-inayopakia kontaina ikisimamiwa na wadenmark,imeshawasili bandarini Mombasa, nchini Kenya.