1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majenerali wa jeshi la Israel wazidi kukosolewa.

Mohammed AbdulRahman16 Novemba 2006

Jeshi la Israel linakabiliwa na mgogoro wa kushuka kwa haiba na sifa kuwahi kuonekana kwa miongo kadhaa, huku majenerali wakijiuzulu kutokana na vita vya Lebanon na harakati za kijeshi huko Gaza, baada ya hujuma za mizinga kuwauwa raia 19 wakipalestina wasio na hatia.

https://p.dw.com/p/CHL8
Wanajeshi wa Israel katika moja wapo ya harakati zao nchini Lebanon dhidi ya Hezbollah mwezi Julai.
Wanajeshi wa Israel katika moja wapo ya harakati zao nchini Lebanon dhidi ya Hezbollah mwezi Julai.Picha: AP

Utafiti wa kura ya maoni mwezi huu umeashiria kwamba nusu ya waisraili wanahisi jeshi linatoa usalama wa kiwango fulani tu na nusu ya waliojibu masuali katika utafiti huo wana shaka shaka kama kweli jeshi la nchi hiyo lina sifa ile ile iliokua ikijivunia mbele ya raia miaka mingi iliopita.

Utafiti uliofanywa na taasisi inayoongozwa na jenerali mmoja maarufu wa jeshi la akiba, ni kinyume na utafiti wa wapo nyuma ulioonyesha kwamba jeshi linaungwa mkono na wengi, ambapo wanaolitumikia wengi ni wanawake na wanaume wa zaidi ya miaka 18.

Wataalamu wanadokeza kwamba kuna hali ya kushuka kiwango cha wanajeshi wenye ujuzi, kinyume na ilivyokua ikionekana zamani, na kwamaba wengine hata hufikiria mara mbili kama kweli ni jambo la muwafaka kutumika jeshini chini ya mpango wa ujenzi wa taifa., huku vijana wakitoa sababu za afya na za kidini.

Mchambuzi wa masuala ya kijseshi kutoka chuo kikuu cha Bar Ilan karibu na Tel Aviv, Stuart Cohen, anasema kwamba heshima ya raia kwa wanajeshi na shauku zimeshuka na hali hiyo imejitokeza zaidi tangu liliposhindwa kuwaangamiza wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon wakati wa vita vaya siku 34 mwezi Julai na Agosti.

Licha ya kwamba jeshi la Israel linaangaliwa kuwa ndilo lenye ngumu kabisa katika Mashariki ya kati, pamoja na hayo limepoteza mikakati ya kupambana na wanaharakati wa Kipalestina na zaidi hivi karibuni na wapiganaji wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon.

Malalamiko ya raia na ukosoaji yalimlazimisha Meja Jenerali Udi Adam aliyeongoza harakati katika uwanja wa kaskazini dhidi ya Hezbollah ajiuzulu mwezi uliopita baada ya vita kumalizika kwa makubaliano ya kusimamisha mapigano katikati ya Agosti. Naye Brigedia Jenerali Gal Hirsch, kama wa kikosi cha wanajeshi katika mpaka na Lebanon akajiuzulu wiki hii. Alijuizulu baada ya uchunguzi kueleza kwamba kukamatwa na kuzuiliwa wanajeshi wawili wa Israel na Hezbollah Julai 12 kungeweza kuepushwa. Kukamatwa kwao kukazusha vita ambapo kiasi ya walebanon 1,200 na waisraili 157 waliuwawa. Mbali na majenerali lawama zimeelekezwa apia kwa waziri mkuu Ehud Olmert.

Jeshi la Israel likakumbwa na malalamiko makubwa zaidi hivi karibuni baaada ya hujuma zake za mizinga kuwauwa raia 19 wakipalestina wiki iliopita katika mji wa kaskazini mwa Gaza wa Beit hanoun, wakiwemo wanawake na watoto waliokua wamelala. Serikali ikaomba radhi ikisema lilikua kosa la kiufundi baada ya makombora kukosa shabaha na kwenda kombo.

Kutokana na hali hiyo kwa jumla maelfu ya wanajeshi awa akiba, uti wa mgongo wa jeshi la Israel waliandamana wakilalamika juu ya uhaba wa mahitaji, ukosefu wa mafunzo na hali isiyoeleweka panapohusika na mikakati katika uwanja wa mapambano wakati wa vita.