1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya umoja wa Ulaya yavamia nyumba ya familia ya Karadzic

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVZx

Pale , Bosnia.

Majeshi ya umoja wa Ulaya na yale ya umoja wa NATO katika mji wa Pale nchini Bosnia yamevamia nyumba za familia na wasaidizi wanaohusika na mtuhumiwa wa uhalifu wa kivita anayetafutwa Radovan Karadzic. Msemaji wa majeshi ya umoja wa Ulaya amesema kuwa majeshi hayo ya kimataifa yanakusanya taarifa juu ya alipo Karadzic . Walimhoji mke wa kiongozi huyo wa Bosnia pamoja na mtoto wake wa kike mapema leo. Karadzic na mkuu wake wa zamani wa majeshi, Ratko Mladic , wamekuwa wakijificha kutokana na kushtakiwa katika mahakama ya umoja wa mataifa ya uhalifu wa kivita kwa muda wa miaka zaidi ya 12.

Watu hao wawili wanakabiliwa na madai ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki kwa kushiriki kwao katika vita vya Bosnia.