1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO : Depo la silaha laripuka na kuuwa 13

23 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGS

Takriban watu 13 wameuwawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa wakati ghala ya silaha iliporipuka karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo hapo jana.

Miripuko kadhaa imetokea karibu na kitongoji cha Magoanine wakati wa magharibi kwenye viunga vya mji mkuu wa Msumbiji Maputo na kuzusha hofu kwenye mji mkuu huo.

Silaha zilizokuwa zikiripuka kwenye depo hilo ziliripuwa zile zilioko karibu na nazo na kusababisha miripuko kadhaa ambayo imekwenda kutuwa kwenye nyumba zilioko karibu na kuziteketeza kadhaa.

Idadi ya vifo inatazamiwa kuongezeka.