1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kimya kuhusu uwezekano wa uchaguzi wa Pakistan kuahirishwa

30 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Chz2

Marekani imekataa kusema lolote juu ya uwezekano wa Pakistan kuahirisha uchaguzi uliopangwa kufanywa tarehe 8 mwezi ujao wa Januari, kufuatia mauaji ya waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto.

Msemaji wa rais George W Bush, Tony Fratto, amesema wapakistan wanatakiwa waamue wenyewe kulingana na hali ilivyo nchini humo baada ya kuuwawa kwa Benazir Bhutto.

Aidha msemaji huyo amesema uchaguzi huo unatakiwa uwe huru na wa haki na wagombea wanatakiwa waweze kuendesha uchaguzi kwa uwazi.

Tume ya uchaguzi nchini Pakistan imesema itafanya mkutano wa dharura hapo kesho Jumatatu kujadili uwezekano wa kuuahirisha uchaguzi kwa sababu ya vurugu zilizosababishwa na kifo cha Benazir Bhutto aliyeuwawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na mtu wa kujitoa muhanga maisha wakati alipokuwa akiondoka kutoka mkutano wa kampeni.

Watu takriban 30 wameuwawa na wengine 53 wamejeruhiwa kufuatia machafuko yaliyozuka nchini Pakistan tangu kuuwawa kwa Benazir Bhutto.