1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa makubwa yakutana Berlin kuhusu Nuklia na Iran

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cw70

BERLIN:

Mataifa makubwa yanakutana mjini Berlin kujadili uwezekano wa kuiwekea vikwazo zaidi Iran kuhusiana na mpango wake tatanishi wa Nuklia.Kabla ya mkutano wa mataifa wa mataifa matano ya kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa,pamoja na Ujerumani, Berlin ilikuwa imetoa mwito wa kupatikana kwa msimamo wa pamoja ili kukabiliana dhidi ya mahitaji ya Iran ya kumiliki Nuklia.Wazir wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani-Frank Walter Steinmeier amesema kuwa ana matumaini kuwa mkutano utaza matunda yanayotarajiwa. China imeonya kuwa mgogoro kuhusu Nuklia na mataifa ya magharibi umefikia kipindi muhimu.lakini kwa wakati huohuo Urusi na China ambazo zote zina maslahi ya kiuchumi na Iran,zinapinga vikwazo zaidi na zinataka kufanyika mazungumzo zaidi.Marekani,Uingereza Ufaransa na Ujeruamni zinataka mbinyo zaidi kwa tehran ili kufunga vinu vyake vya Nuklia ambavyo zinashuku kuwa vinanuiwa kutengeneza silaha za Nuklia.