1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa yakubaliana kuanza majadiliano.

16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcDu

Bali.

Serikali za mataifa kadha duniani kote zimefurahia makubaliano ya kuanza majadiliano kwa ajili ya mkataba mpya wa hali ya hewa utakaokuwa badala ya ule wa Kyoto. Wajumbe kutoka mataifa 190 katika mkutano uliotayarishwa na umoja wa mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa katika kisiwa kilichoko nchini Indonesia cha Bali wamefanikiwa kupata makubaliano baada ya wiki mbili za majadiliano makali. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa makubaliano hayo ni ushahidi kuwa mataifa yote yanatambua hatari ya suala hili. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameusifu msimamo wa pamoja wa mataifa ya Ulaya. Merkel pia amesema kuwa licha ya kuwa njia ya kupata mkataba utakaokuwa badala ya ule wa Kyoto ni ngumu, madaraka yaliyoidhinishwa na makubaliano ya Bali ni muhimu.

Utawala wa Marekani umeeleza wasi wasi wake kuwa waraka wa mwisho haukuweza kuelezea vya kutosha majukumu ya upunguzaji wa gesi zinazochafua mazingira kwa mataifa yanayoendelea.

Wakijibu shutuma hizo za Marekani mwakilishi kutoka Papua New Guinea amesema.

Nataka kuiuliza Marekani , tunaomba uongozi wenu, tunahitaji uongozi wenu, lakini iwapo kwea sababu fulani hamko tayari kuongoza, tuachieni sisi wenyewe. Tafadhalini jiondoeni msituzuwia njia.

Makundi ya ulinzi wa mazingira yamesema kuwa makubaliano hayo yanakosa uwezo kamili.