1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini kuhusu mgogoro wa madereva wa treni Ujerumani

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJKp

Majadiliano ya ngazi ya juu yanatazamiwa kufanywa siku ya Jumanne kati ya chama cha wafanyakazi cha madereva wa treni-GDL na shirika la reli-Deutsche Bahn.Waziri wa usafiri wa Ujerumani Wolfgang Tiefensee amesema,ana hakika kuwa pendekezo jipya la Deutsche Bahn litafungua njia ya kuanzishwa majadiliano mapya,kati ya pande hizo mbili.Hapo awali,mkuu wa GDL bwana Manfred Schell alidai ongezeko la mshahara la asilimia 15.