1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

mawaziri wa nje Umoja wa Ulaya

28 Machi 2008

Mawaziri wa nje wa UU wakutana Slovenia kuzungumzia kususia au la ufunguzi wa Olimpik Beijing August 8,mwaka huu.

https://p.dw.com/p/DWfy
Angela MerkelPicha: AP

Mawaziri wa nje kutoka nchi 27 zanachama wa Umoja wa Ulaya wanajadiliana hii leo huko Slovenia jibu gani watoe kwa mkomoto unaoendeshwa na China huko Tibet.Wakati wa siku 2 hizi za mazungumzo yao leo na kesho watazinagatia pia iwapo waitikie vilio vya kususia alao sherehe za ufunguzi za michezo ya Olimpik ya Beijing,August,mwaka huu.

►◄

Kabla kuanza kikao cha leo huko Slovenia,mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya, waziri wa nje wa Ujerumani Frank-walter Steinmeier,alibainisha wazi kwamba si kanzela Angela Merkel wala yeye wanaopanga kuhudhuria sherehe ya ufunguzi ya michezo ya mwaka huu ya Olimpik mjini Beijing,China.Alisema lakini,hatua hiyo haihusiani na visa vya Tibet.

Akiwasili huko Brodo pri Kranju,kaskazini mwa mji mkuu wa Slovenia -Ljublijana,Bw.Steinmeier alisema kutohudhuria sherehe za ufunguzi hakuna maana Ujerumani inaigomea michezo ya Olimpik nchini China kutokana na mkomoto wa china huko Tibet.

Akaongeza waziri wa nje wa Ujerumani,

"Situmai waziri wa michezo wa Ujerumani (Bw.Wolfgang Schauble) anapanga kuhudhuria wala Kanzela au hata mimi."

Mawaziri wa nje wa UM kwahivyo watapeana hoja zao wale wanaopendelea kuisusia michezo hiyo na wale wasioungamkono -mfano wa Uingereza-mwenyeji wa michez0 ya Olimpik 2012 baada ya Beijing.

Lakini, viongozi kadhaa wa Ulaya ya mashariki waliojiunga na UU baada ya miongo kadhaa nchi zao kutaliwa na ukoministi,wanapanga kukaa kando ya sherehe za ufunguzi.

Rais wa Jamhuri ya Czech Vaclav Klaus na mwenzake wa Estonia Toomas Hendrik Ilves pamoja na waziri mkuu Donald Tusk wamearifu hawaendi Beijing.

Mawaziri wa nje wa danmark na Cyprus pia wamesema wanapinga vilio vya kuisusia michezo ya Beijing kama waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.

"Swali la Olimpik lisichanganywe kamwe na siasa,kwani haya ni maswali 2 tofauti."alisema waziri wa nje wa Cyprus Markos Kyprianou.

Akikabiliwa n a mfarakano huu wa msimamo miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya, rais wa Ufaransa Nocolas Sarkozy ,aliekutana na waziri mkuu Brown jana mjini London,amesema atawauliza viongozi wa UU kabla kuanza michezo hiyo iwapo wanataka kususia ufunguzi wa michezo.Sarkozy alisema kwamba hakuna hata mwanachama mmoja kati ya wote 27 alietoa mwito kuisusia michezo ya beijing.

Rais wa Ufaransa aliongeza lakini kwa jicho la sura ya mambo ilivyo hivi sasa ,anabakisha haki yake kusubiri kuamua atakwenda au hataenda kwenye ufunguzi wa michezo.

Wakati inatazamiwa mjadala huu juu ya china na Olimpik kupambamoto,mawaziri wa nje wa Ulaya wanaafikiana kwa jumla kuwa Beijing ianzishe mazungumzo na Dalai Lama ,kiongozi wa waumini wa madhehebu ya Budha huko Tibet aishie uhamishoni nchi za nje.

Maandamano ya kupinga utawala wa China huko Tibet,yalianza hapo machi 10 mjini Lahsa, mji mkuu wa Tibet kukumbuka wa uasi wa 1959 dhidi ya utawala wa China.Ni kisa hiki kilichoongoza kwa Dalai lama, kiongozi wa watibet kuihama nchi na kukimbilia India.

Kuhusu russia, kikao hiki cha mawaziri wa nje huko Slovenia, kitaandaa msingi kwa mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika mjini Moscow majira haya ya kiangazi kuhusu ushirika katika pande mbali mbali kati ya Russia na UU.

UU unatumai kushika madaraka huko Moscow kwa Dmitri Medvedev kunaweza kukaimarisha usuhuba kati yao na Russia-usuhuba uliotetereka chini ya rais wa zamani Vladmir Putin.