1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Nje wajadili upanuzi wa NATO

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJt0

BRUSSELS:

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Kujihami ya Magharibi-NATO wanakutana mjini Brussels kujadili upanuzi wa jumuiya hiyo.Albania,Croatia na Macedonia hivi karibuni zinatazamiwa kualikwa kuwa wanachama katika NATO.Ugiriki lakini imeonya kuwa itapinga uanachama wa Macedonia.Serikali ya Athens ina hofu kuwa Macedonia huenda ikadai kuwa ina mamlaka katika eneo la Ugiriki ambalo pia huitwa Macedonia.

Mgogoro mwengine unahusika na suala iwapo NATO iifungue mlango kuzikaribisha Georgia na Ukraine,nchi ambazo hapo awali zilikuwa sehemu ya Soviet Union ya zamani.