1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa fedha wa Ugiriki

4 Oktoba 2011

Ugiriki huenda ikalazimika kusubiri hadi kati kati ya mwezi ujao kuweza kupatiwa fungu jengine la mkopo wa Euro bilioni nane.

https://p.dw.com/p/12lHP
Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble kulia) akizungumza na waziri mwenzake wa Ubeligiji Didier ReyndersPicha: dapd

Mawaziri wa fedha wa nchi za eneo la sarafu ya Euro wamekubaliana jana usiku mjini Luxembourg wasubiri kwanza kabla ya kupitisha uamuzi wao.Wanasubiri kuona ripoti ya tume ya pande tatu inayozileta pamoja Umoja wa Ulaya, benki kuu ya Ulaya na shirika la fedha la kimataifa, IMF. Hali hiyo haimaanishi lakini kwamba Ugiriki haina uwezo wa kulipa madeni yake.

Kimoja ni dhahiri: Ugiriki haitoweza kupunguza nakisi ya bajeti yake kwa kiwango kikubwa kama ilivyoahidiwa hapo awali. Serikali ya Ugiriki tayari imeshaungama. Nae kamishna wa Umoja wa Ulaya anaeshughulikia masuala ya sarafu, Olli Rehn, akawaarifu mawaziri wa umoja wa sarafu ya Euro mara tu mkutano wao ulipoanza :

"Yadhihirika kana kwamba Ugiriki haitalifikia lengo lake mwaka huu."

Ikiwa Ugikiri itashindwa kuyafikia malengo yaliyowekwa ambayo ni pamoja na kupunguza nakisi ya bajeti yake, huenda basi fungu jengine la mkopo lisitolewe. Hayo yalisemwa pia na waziri wa fedha wa serikali kuu ya Ujerumani Wolfgang Schäuble aliyesisitiza, hata hivyo, hakuna bado kilichoamuliwa, wanasubiri ripoti ya tume ya pande tatu inayozileta pamoja Umoja wa Ulaya, Benki kuu ya Ulaya na shirika la fedha la kimataifa, IMF.

Flash-Galerie Griechenland Athen Proteste vor dem Parlament
Maaandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu mjini AthensPicha: dapd

Wakati huo huo, maandamano yanaendelea nchini Ugiriki. Watumishi wa serikali wamezifunga hii leo njia za kuingilia katika wizara za fedha, kilimo na wizara nyengine kadhaa mjini Athens wakilalamika dhidi ya hatua za kufunga mikaja wanazohoji zinaukaba uchumi wa nchi hiyo.

Maandamano haya yanatokea mnamao mkesha wa mgomo jumla wa masaa 24 ulioitishwa na shirika linalopigania masilahi ya wafanyakazi wa mashirika ya umma na yale ya kibinafsi.

"Watu wameingiwa na wasi wasi mkubwa na kukasirika sana" , amesema hayo Ilias Iliopoulos ambaye ni katibu mkuu wa shirika linalopigania masilahi ya watumishi wa mashirika ya umma-Adedy- anaeshiriki katika maandamano mbele ya wizara ya fedha.

"Maandamano ya leo yanahusiana na sheria za kazi. Lakini kuna bajeti mpya inayoashiria hatua ziada za kufunga mkaja-",ameongeza kusema Ilias Iliopoulos.

Griechenland Finanzkrise Evangelos Venizelos Finanzminister in Athen
Waziri wa fedha wa Ugiriki Evangelos VenizelosPicha: dapd

Mawaziri wa fedha wa nchi za eneo la sarafu ya Euro wametangaza jana Athens inaweza kusubiri hadi kati kati ya mwezi wa November mwaka huu kuweza kupata fungu jengine la mkopo wenye thamani ya Euro bilioni nane.

Muda huo unaweza ukatumiwa na tume ya pande tatu ili kuzidi kuishinikiza Ugiriki isawazishe mgogoro wake wa madeni.

Waziri wa fedha wa Ugiriki anatazamiwa kuzungumza na waandishi habari muda mfupi kutoka sasa.

Mwandishi:Hasselbach ,Christoph(DW Brüssel)/Hamidou Oummilkheir/Reuters

Mhariri: Miraji Othman