1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa msikiti waendelea nchini Pakistan

6 Julai 2007

Katika mvutano wa msikiti nchini Pakistan majeshi ya usalama ya nchi hiyo yameimarisha shinikizo dhidi ya wanaitikadi kali wa kiislamu.

https://p.dw.com/p/CB31
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan
Rais Pervez Musharraf wa PakistanPicha: AP

Wakati huo huo rais Pervez Musharraf ameyataka majeshi hayo yawe na subira.Mvutano baina ya wanaitikadikali wa kiislamu na majeshi ya Pakistan umeendelea kushtadi kwenye msikiti mwekundu, Lal masjidi mjini Islamabad.

Majeshi yameimarisha shinikizo dhidi ya watu hao wakati rais Musharraf ameyataka majeshi hayo yafanye subira ili kuwawezesha wanawake waliomo msikitini humo kuondoka.Rais Musharraf ameyaambia majeshi yake yasimamishe mashambulio kwa muda.

Lakini habari zinasema kuwa naibu kiongozi wa msikiti huo Ghazi Abdu Rashid hataki kusalimu amri. Amesema kuwa yeye na wafuasi wake wanastahabu kifo kuliko kusalimu amri.

Hadi sasa watu 19 wameshakufa kutokana na mvutano huo ambapo wanaitikadi kali wa kiislamu wanapigania sheria za kiislamu . Watu hao wanataka sheria hizo zitumike katika mji wa Islamabad.

AM