1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa reli

3 Julai 2007

Mogomo wa madereva wa reli na mkutano wa 3 wa kilele juu ya nishati katika afisi ya Kanzela ndio mada 2 kuu zilizojadiliwa na wahariri leo hii:

https://p.dw.com/p/CHSX

WIESBADENER KURIER linajishughulisha na madai ya vyama vya wafanyikazi:Laandika:

“Hadi sasa majadiliano kati ya shirikisho la vyama vya wafanyikazi wa reli na waajiri-shirika la reli, yamekiuka mpaka kwa kila upande:Madai ya nyongeza za mishahara yamevuka mpaka katika kila aina ya ajira kati ya nyongeza ya 7% na 31%.Yamevuka mpaka pia juu ya silaha zinazotumika katika vita hivi.Baada ya kutonesha kidonda kidogo-kidogo, madereva wa treni wagoma na abiria wateseke.”

Mod.Ni maoni ya WIESBADENER KURIER.

Ama gazeti la MÄRKISCHE ALLGEMEINE kutoka Potsdam lionatupa jukumu mabegani mwa viongozi wa shirika la reli:

“Tuhuma za shirika la reli la Ujerumani “Deutschen Bahn” kwamba shirikisho la wafanyikazi linaendesha mgomo wake mgongoni mwa abiria –wateja wake-azma yake ni dhahiri kabisa.

Mgomo wa reli unawaathiri abiria moja kwa moja kinyume na mgomo viwandani.Endapo shirika la reli kweli likitaka kuwaondoshea adha abiria wake,basi lingejitolea kuwanyoshea mkono mpya wa maridhiano wafanyikazi na kuwarejesha katika meza ya mazungumzo.”

Ni maoni ya MÄRKISCHE ALLGEMEINE kutoka Potsdam.

Gazeti la KÖLNISCHE RUNDSCHAU kutoka mjini Cologne linalitaka shirika la reli kutowaonea wafanyikazi wake.Lasema:

”Mkuu wa shirika la reli la Ujerumani, Mehdorn hivi sasa haachi nafasi ya kulipigia upatu shirika lake kuwa linaenda uzuri kiuchumi.Na ukweli wa mambo, limejipatia faida nono kuvunja rekodi.

Mwaka uliopita lilivuna faida ya Euro bilioni 1.7 na siku zake za usoni zinanawiri tena kwa kipindi kirefu kijacho.Kuongeza mishahara mara 2 kwa kima cha 2% katkka kipindi cha miaka 2 si kima kisichomudu kuongezwa.”

Likigeuza mada gazeti la BERLINER ZEITUNG lajishughulisha na jinsi ya kuhakikisha matumizi ya nishati siku zijazo.Mada hii yaendelea kuzusha mabishano.Kikao cha jana katika afisi ya kanzela- cha tatu cha aina hii- kilikua na azma ya kusaka jibu.Gazeti lauliza:

“ Kwanini kila mara sera za nishati za serikali ya Ujerumani na viwanda vya nishati hugongana na kuzusha mvutano ?

Je, hii yatokana na kujifikiria binafsi makampuni ya nishati ? Jibu ni ndio.Hakuna tawi jengine lolote la viwanda vya Ujerumani linapokabiliana na serikali linajihisi lina nguvu m no kama viwanda vya nishati.Viwanda vya nishati vina mtandao mkubwa kumudu kuwashawishi wanasiasa kurudhia vitakavyo.”

Ni maoni ya BERLINER ZEITUNG.

Likitukamilishia mada hii ya nishati ,gazeti la LANDESZEITUNG kutoka Lüneburg laandika:

“Uamuzi wa kuachana na vinu vya nishati ya kinuklia kwa kweli unaigawa serikali ya muungano ya Ujerumani.Ushindi wa vyama vya kihafidhina utabadili uamuzi huo.Siku za mbele hali itakua vyengine kabisa .Viwanda vya nishati inapangwa kuvijumuisha na mkakati wa siku zijazo ingawa kufanya hivyo vitapoteza tu nafasi zao.Tangu mpango wa kupunguza matumizi ya nishati hata ushindani kutoka nishati ya kimazingira kutayaopunguzia faida.Tunaamini kwahivyo, makampuni makubwa ya mafuta yatabidi kuyafungulia mlango yale ya nishati inayoweza kupatikana tena na tena.