1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa wafanyakazi wa serikali umeingia siku ya pili leo

Josephat Nyiro Charo19 Agosti 2010

Polisi wametumia risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji

https://p.dw.com/p/Oro4

Wafanyakazi wa serikali nchini Afrika Kusini wameendelea na mgomo wao kwa siku ya pili hii leo. Polisi wamelazimika kutumia risasi za mpira kuwatawanya waalimu waliokuwa wakirusha matofali na mawe. Wakati huo huo wauguzi wamelivunja lango la hospitali moja mjini Johanneburg kwenye mgomo huo wa nchi nzima wa wafanyakazi wanaodai kuongezwa mishahara. Josephat Charo amezungumza na bwana Isaac Khomo, mwandishi wa habari mjini Johannesburg na kwanza kumuuliza hali ilivyo kwa sasa.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri:Abdul-Rahman