1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 100 korokoroni kwa mwanajeshi wa kimarekani

23 Februari 2007

Hukumu ya kifungo cha miaka 100 gerezani imetolewa kwa sergeant Coretz kwa kuimbaka msichanwa miaka 14 wa kiiraki na kuuhilikisha ukoo wake mzima.

https://p.dw.com/p/CHJP

Mwanajeshi wa kimarekani-Sergeant Paul Cortez,mwenye umri wa miaka 24 alihukumiwa jana huko Fort Campbell,Kentucky, kifungo cha miaka 100 korokoroni kwa mchango wake katika kumbaka na baadae kumuua msichana wa miaka 14 wa kiiraqi na kuuhilikisha ukoo wake mzima nchini Iraq.

Sergeant Coretz aliungama mahkamani kwamba alikua miongoni mwa wanajeshi 5 wa kimarekani waliopanga njama ya mwezi Machi,mwaka jana ya kubaka na kuua huko Mahmudiyah,kusini mwa mji mkuu Baghdad wakati wakinywa pombe ya gin na whiski na kucheza karata kwenye kituo cha kukagua misafara ya magari.

Alitaka radhi kwa ndugu zake 2 wakiume na kwa wazee wake waliokuwapo mahkamani.

Sergeant Cortez akichururikwa na machozi wakati askari wenzake wa kikosi cha wanahewa 101 wakitoa ushahidi kwa niaba yake kabla hakupitishiwa adhabu.Akanukuliwa kuwaambia, “nawependa wenzangu na nasikitika kwa maovu niliyotenda.” Mwisho wa kumnukulu.

Coretz amekutikana na hatia ya kupanga njama ya kubaka,na halafu kutekeleza kitendo hicho cha ubakaji,kesi 4 za kuua pamoja na mashtaka mengine pamnoja na kukiuka amri inayokataza kunywa pombe akiwa kazini.

Coretz alikuwa mwanajeshi wapili kuungama hatia katika kesi hiyo iliogonga vichwa vya habari na kuhanikiza-moja kati ya visa vingi vilivyochafua na kutia dosari heba ya wanajeshi wa kiarekani nchini Irak.

Hakimu wa mahkama ya kijeshi huko Kentucky, awali alimhukumu sergeant Coretz kifumngo cha maisha bila ya msahama na akimaliza kifungo asitolewe kwa hishima.

Baadae kufuatia maafikiano yaliofikiwa na kamanda wake mshtakiwa ,ilionekana apewe kifungo cha miaka 100 korokoroni –kifungo ambacho baada ya miaka 10, aweza kusamehewa na kutoka gerezani.

Kesi hii iliwastusha watu wengi kuona wanajeshi wanapanga njama bila kujali kumuingilia kwa nguvu msichana wa miaka 14 waliemuona akitembea njiani katika kijiji cha Irak na wakajaribu makusudi kuficha madhambi yao kwa kuiteketeza familia yake nzima msichana huyo na kuitia moto nyumba yao.

Katika taarifa ambayo mara kwa mara ikikatizwa kwa vilio,sergeant Coretz, alisimulia vipi mwanajeshi mwenzake alimdhibiti mtoto huyo wa kike wa kiraqi sakafuni wakati yeye akimuingilia kwa nguvu.

Wanajeshi wengine 2 wa kimarekani wanasubiri hukumu zao wakati mshtakiwa wa 5 anaetuhumiwa ni kiongozi wa gengi hilo-Steven Green,aliefukuzwa jeshini kabla kisa hiki kufichuka hadharani, atahukumiwa mbele ya mahkama kuu ya shirikisho hapo baadae.