1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjadala juu ya Jeshi la Ujerumani Afghanistan

7 Aprili 2010

Je, Bundeswehr linapata mafunzo na silaha za kutosha ?

https://p.dw.com/p/Mp1w
Jeshi la Ujerumani(Bundeswehr)Picha: AP

Baada ya mapigano makali Ijumaa iliopita ya pasaka karibu na Kundus, nchini Afghanistan,ambamo wanajeshi 3 wa Ujerumani waliuwawa ,mjadala umepambamoto nchini Ujerumani, kuhusu mafunzo ya wanajeshi wake na silaha wanazopatiwa .Swali linaloulizwa ni je, wanajeshi wa Bundeswehr nchini Afghanistan, wana kila zana wanazohitaji kwa vita dhidi ya watalibani ? Katika swali hili, maoni yanatofautiana.

Mjumbe anaeondoka madarakani mwenye jukumu la kushughulikia masilahi ya wanajeshi Reinhold Robbe kutoka chama cha Upinzani cha SPD, ametaja kasoro kadhaa tangu katika utoaji mafunzo na hata katika kuwapatia zana za silaha.Wanajeshi 3 waliouwawa walikuwa askari wa miavuli kutoka kambi ya Seedorf,kikosi ambacho mjumbe huyo alikitembelea muda mfupi kabla ya kupelekwa Afghanistan.Alipotembelea huko, wanajeshi walilalamika kwamba, hawakuwa na magari ya kutosha ili kufanyia mazowezi watakapojikuta kwenye mapigano-aliarifu Bw.Robbe katika mahojiano yake na gazeti moja.

Hivyo, mjumbe huyo anaeshughulikia wanajeshi, amekariri kile alicholalamika ndani ya ripoti yake ya mwaka. Alisema hakuna magari ya kutosha chapa "DINGO" na "DURO" kwa mafunzo ya madereva wa magari ya kijeshi nchini Ujerumani.

Mwanasiasa mwengine amesisitiza dai lake kuwa, Jeshi la Ujerumani linahitaji haraka mno helikopta za kivita kwa matumizi nchini Afghanistan pamoja na zana za kisasa za kukagua hali ilivyo katika medani ya vita.

Mwanasiasa wa chama cha CVDU Ruprecht Polenz,haelewi kwanini.Anasema kwamba, wanasiasa hawapasi kujigeuza ndio maamirijeshi na kwamba, wanapaswa kutegemea hukumu zinazopitishwa na wanajeshi.Mwenyekiti huyo wa Halmashauiri ya siasa za nje Bungeni Ruprecht Polenz, anasema:

"Sina taarifa kwamba , kuna maombi maalumu ya Jeshi la Ujerumani kwa matumizi yao nchini Afghanistan, ambayo hayakutekelezwa.Nionavyo mimi , tumewapatia wanajeshi zana za kutosha na tumewapa mafunzo mazuri kwa jukumu lao,ama sihivyo, isingekuwa dhamana kufanya hivyo."

Inspekta mkuu wa zamani wa Jeshi laUjerumani,Herald Kujat, amekosoa kuwa wanajeshi wa Ujerumani, wamepungukiwa huko Afghanistan na zana za kisasa za kuikagua hali ya mambo vitani.Ni kutokana na sababu kama hiyo , ndipo Ijumaa ya pasaka iliopita, wanajeshi wa Ujerumani walijikuta katika mapigano makali na watalibani.

Wizara ya ulinzi ya Ujerumani, inakanusha kabisa tuhuma hizo.Inadai kwamba, Bundeswehr au jeshi la Ujerumani, limejizatiti barabara kisilaha na kwamba, lililikagua eneo hilo ambako mapigano yalitokea.

Inspekta-mkuu Volker Wieker, alieleza kwanini wanajershi waliokuwa aridhini hawakuweza kupatiwa msaada wa hujuma za mabomu kutoka hewani : Palitumika tu ndege zilizoruka karibu sana na aridhini bila ya kutumia silaha kwa sababu pakihofiwa kuhatarisha wanajeshi na raia.Tangu ile hujuma iliokwenda kombo Septemba mwaka jana, Jeshi la Ujerumani, katika kugutuka tu kushambulia kutoka hewani, limekuwa likisitasita.

Mwandishi: Werkhäuser,Nina (DW Berlin)

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Uhariri: Abdul-Rahman