1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjane na wana watano wa Pinochet wazuiliwa

Jane nyingi5 Oktoba 2007

Maafisa wakuu nchini Chile wamemtia mbaroni mjane na watoto watano wa aliyekuwa rais wa Chile Agosto Pinochet kwa jukumu lao katika wizi wa mamilioni ya dolla ambazo wameficha katika akaunti zao nchini marekani.

https://p.dw.com/p/C7iY
Jacqueline Pinochet, mtoto wa marehemu Agosto Pinochet akiwasili katika makao makuu ya polisi mjini Santiago
Jacqueline Pinochet, mtoto wa marehemu Agosto Pinochet akiwasili katika makao makuu ya polisi mjini SantiagoPicha: AP

Ni tangazo lilopokelewa kwa hisia mbalimbali nchini Chile hali inayodhihirisha mgawanyiko uliko hadi sasa miongoni mwa wachile karibu miezi 10 baada ya kufariki kwa Pinochet akiwa na umri wa miaka 91. Baadhi yao waliamua kufanya maandamano kupiga uamuzi huo huku wengine wakinywa vileo na kuimba nyimbo za kizalendo kukaribisha kutiwa mbaroni kwa Bi Hiriart na wanawe watano.

Punde baada ya kukamtwa kwa Bi Hiriat wa umri wa miaka 87 alikimbizwa katika hospitali ya kijeshi ya Santiago kutokana na shinikizo la damu mwilini. Waziri wa sheria Carlos Maldonado amesema familia ya marehemu Pinochet haitapewa aiana yeyote ya matibabu maalum kwa kuwa Wachile wote wako sawa kulingana na sheria.

Jaji Carlos Cerda alitoa agizo la kutiwa mbaroni kwao baada ya kubainika kuwa walishiriki katika uhalifu huo.Hata hiyo mjane wa pinochet na mmoja wa wanawe waliwasilisha malalamishi mahakamani wakidai agizo hilo lilikuwa kinyume cha sheria. Jaji Cerda pia ameagiza kutiwa mbaroni kwa watu wengine 17 wakiwemo waliokuwa wasaidizi na mawakili wa kiongozi huyo aliyetajwa na wengi kuwa dikteta.Miongoni mwao ni aliyekuwa msemaji wake Guillermo Grain na wakili Gustavo Collao

Jaji huyo ndiye anasimamia kesi hiyo ambayo Marehemu Pinochet, yadaiwa aliimba zaidi ya dolla millioni 25 za Chile na kuzipeleka kisiri nchini marekani kwa usaidizi wa benki ya Riggs iliko mjini Washinton Marekani. Kashfa hiyo ilichipuka mwaka 2004 baada ya uchunguzi na bunge la marekani kubaini mamia ya akaunti katika jina la marehemu Pinochet na jamaa zake katika benki hiyo ya Riggs.

Wabunge wa chama cha kikomunisti kilichopigwa marufuku wakati wa utawala wa kijeshi kilikaribisha hatua ya kutiwa mbaroni kwa mjane wa Pinochet na wanawe watano.Pinochet ambaye utawala wake kati ya mwaka 1973 na 1990 ulihusisha kunyanywa na kuwauawa kwa maelfu ya watu walifariki december mwaka jana kutokana na maradhi ya moyo.

Alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani wakati huo.Kifo chake kilitamatisha juhudi za miaka mingi za kumfungua mashtaka kutokana na kuwaua wapinzani wake na wizi wa pesa za serikali wakati wa utawala wake wa kijeshi. Alikwepa mashtaka hayo baada ya mawakili wake kudai kuwa kutokana na ugonjwa aliokuwanao wa akili hawezi kujitetea.

Hata hivyo Ufaransa inanuia kuwafungulia mashtaka washirika 17 wa marehemu Pinochet kutokana na kupotea kwa wafaransa wanne katika miaka ya 70.