1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mkuu wa Fatah

7 Agosti 2009

Saudi Arabia yawaonya wapalestina waache magombano.

https://p.dw.com/p/J5Ud
Mahmoud AbbasPicha: AP

Mkutano wa kwanza mkuu wa chama cha ukombozi wa Palestina - FATAH- tangu kupita miaka 20, uliendelea jana na misukosuko yake.Wapenda-mageuzi ndani ya FATAH waliendelea kudai kwa nguvu pawepo mabadiliko katika uongozi wa juu wa chama huku vigogo vya zamani vikibisha kuacha hatamu.

Chini ya hali hii ya mvutano ,Saudi Arabia imewaonya wapalestina kwamba wasitegemee kuundwa kwa dola la Palestina kabla ya kwanza kumaliza mfarakano katii yao.Magombano miongoni mwa wapalestina wenyewe kwa wenyewe na hatari ya kugawanyika kabisa chama cha FATAH cha Rais wapalestina Mahmud Abbas mbalii na uhasama uliopo tayari kati ya FATAH na HAMAS,kumemfanya mfalme Abdullah wa Saudi Arabia Saudi Arabia,kutoa onyo kali lisilo la kawaida kwa wapalestina . Amewaambiia:

"Hata iikiwa dunia nzima imeafiki kuundwa kwa dola huru la kipalestina ,na msaada wote utakaotolewa kufikia shabaha hiyo,dola hilo halitaiiundwa kwa kadiri jumba la wapalestina limegawika wenyewe kwa wenyewe."

Mfalme Abdulla wa Saudia amemuandikia barua wazi rais mahmud Abbas wa Mamlaka ya ndani ya wapalestina.Barua hiyo imechapishwa katika gazeti la kiarabu linalotoka london "Al-Hayat".

Ikiwa mapatano ya amani ya mashariki ya Kati yaweza kujadiliwa ili kuunda dola la wapalestina kandoni mwa lile la waisraeli, basi mapatano hayo yatatiiwa saini na Chama cha Uko mbozii wa Palestina (PLO) kinachotambuliwa na Israel na UM ambamo FATAH ik,iongozwa na Bw.Abbas ina sauti kubwa.

Umoja wa chama cha FATAH kwahivyo ni muhimu sana kufanikisha utaratiibu wa amani.Dola za magharibi nyuma ya Bw.abbas zionatumai kuwa mkutano huu unaoendelea wa chama cha FATAH utarejesha imani kwa FATAH kabla ya uchaguzi unaotazamiwa kufanywa mwakani 2010-mwaka unaoweza kuona mpango mpya wa Marekani wa kuleta ufumbuzi wa amani wa mgogoro wao na Israel.Chama cha FATAH kikitolewa maanani kwa mazungumzo ya muda mrefu na Israel bila kuzaa matunda na ila za rushua wakati wa uongozi wa marehemu Yasser Arafat,

na kuaibishwa na chama cha HAMAS katika uchaguzi uliopita 2006, chama cha FATAH kinahitaji mno kufufuliwa -hii ni kwa muujibu wa kizazi kipya cha vijana wanaolilia mageuzi chamani. Kizazii hicho kinapaza sasa sauti wakati baadhi ya wazee wa chama katika Kamati kuu wakitangaza hawatagombea tena viti vyao. Ni wajumbe 8 kati ya wote 16 wa Halmashauri Kuu ya FATAH wanagombea tena.Wakosoaji lakini wanadai vigogo hivyo vya zamani vinaweza bado kusalia madarakani kwa kuusheheni mkutano huu dakika ya mwisho wafuasi wsao hadii 700.Mchanga kabisa katii yao ana umri wa miiaka 70.

Husam Khader mwenye umri wa miaka 47 amesema angependa sana kugombea kiti katika Kamati kuu ya FATAH,lakini amewatuhumu wanachama wa kamati hiiyo kununua kura na kuwaingiza jamaa zao na watumishi wao kuhudhuria mkutano kama wajumbe.Baadhi ya wajumbe mkutanoni wameripoti patashika kubwa na majadiliano motomoto. kumhsu mjumbe wake mmoja i Mohammed Dahlan.Anasemekana akizungumza jana kwa masaa kadhaa faraghani na mwenyekiti mahmud Abbas: mjumbe mmoja alisema,

"Kuna mzozano mkubwa kumhusu Mohammed Dahlan.Kuna watu wanaomtuhumu Dahlan ndie aliesababisha chama cha FATAH kupoteza madaraka mwambao wa Gaza.Na kuna watu wanaodai sasa Dahlan asiichaguliwe tena kuwamo ndani ya Halmashaurii kuu mnamo miaka 4-5 ijayo."

Halmashauri kuu ya chama cha FATAH, mata ya mwiisho ilichaguliwa mjini Tunis, 1989.Kwa desturi huwa na wajumbe 21.18 kati yao huchaguliwa na 3 huteuliwa.Watano kati yao pamoja na kiongozi yasser Arafat wamefariki tangu uchaguzi wa Tunis.Kuwateua wajumbe wa halmashaurii kuu mpya kulikua kuanze jana jioni na kumalizike leo ijumaa.Uchaguzi uliikua ufanyike kesho.Hakuna anaembisha Kiongozi Mahmud Abbas.

Mwandishi/Ramadhan Ali

Mhariri: M. Abdul-Rahman