1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Bali ulenge kuapta mkataba mpya

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CazJ

BALI:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kukubaliana njia za kupambana na ongezeko la joto duniani, hadi mwishoni mwa mwaka 2009.Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani unaofanywa Bali nchini Indonesia,umependekeza nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda zipunguze uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira kwa asilimia 25 hadi asilimia 40,kama Umoja wa Ulaya na nchi zinazoendelea zinavyotaka.Lakini Japan, Marekani,na Kanada zinapinga.

Katibu Mkuu Ban amesema,kupanga viwango hivyo katika mkutano huo wa Bali huenda ni matumaini makubwa mno.Badala yake ameshauri lengo kuu liwe majadiliano ya kupata mkataba mpya utakaochukua nafasi ya Mkataba wa Kyoto unaomalizika mwaka 2012.