1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G8 ni mafanikio kwa utawala wa Merkel.

Sekione Kitojo8 Juni 2007

Mkutano wa mataifa tajiri yenye viwanda mjini Heiligendamm umemalizika, na matokeo ya mkutano huo wa kiuchumi wa dunia kila mara yanabaki kuwa kazi ya wakubwa na wasaidizi wao. Wanaongoza majadiliano ya mwanzo na kuchambua kwa makini nyanja zote na kisha wanatoa matokeo. Hadi sasa mafanikio yalikuwa katika suala la mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na suala la misaada kwa bara la Afrika ikiwa kwa kiasi kikubwa ni mafanikio kwa utawala wa Angela Merkel.

https://p.dw.com/p/CHCw
Viongozi wa mataifa ya G8 wakichombeza baada ya majadiliano makali. Kushoto ni George W. Bush, Angela Merkel kati, na Vladimr Putin wa Russia.
Viongozi wa mataifa ya G8 wakichombeza baada ya majadiliano makali. Kushoto ni George W. Bush, Angela Merkel kati, na Vladimr Putin wa Russia.Picha: AP

Pamoja na hayo kazi ya kansela Angela Merkel haikuwa rahisi inabaki pale pale na bila jibu.

Bila shaka, kwa kansela Angela Merkel mkutano wa G8 mjini Heilingendam ulikuwa ni wakati nyota yake ilipong’ara katika utawala wake.

Zaidi ya hayo, matokeo ya majadiliano katika duru za viongozi na wakuu wa nchi yanaridhisha, lakini pia sio ndoto zote za kupata mambo mazuri sana juu ya uwajibikaji zimepatikana. Kwa vyovyote vile imeonekana na kila mmoja kuwa kuna maelekezo mazuri, kwa wale walioko mbele wakiwa wanasikitishwa na yale yanayotokea.

Kansela ana kazi nzito mbele yake. Kwa bashasha, umakini na mbinu za majadiliano , ameweza kwa kiasi kikubwa, kuendesha mkutano vizuri.

Rais wa Marekani George W. Bush ameweza kujitoa katika ujinga wa kutojua suala la mabadiliko ya hali ya hewa, waziri mkuu wa Italia Romano Prodi ameweza kuingia katika juhudi mpya , kuhusiana na Afrika , ambapo mwishoni hakuweza kujitoa. Rais wa Urusi Vladimir Putin na rais Bush wa Marekani katika mkutano huu wa Heligendamm walijaribu kutuliza mzuka wao wa vita baridi.

Makubaliano kamili ya kuhakikisha lengo la hali ya hewa linafikiwa bado hayajafikiwa. Lakini hivi sasa kuna msingi wa pamoja , wa uwezekano wa kufanyakazi kwa pamoja. Hili ni jukumu sasa la mawaziri wa wizara za mazingira, kwa kushirikia na utaratibu wa umoja wa mataifa na kufanyakazi katika kupatikana kwa muafaka utakaokuwapo baada ya makubaliano ya Kyoto. Mambo yanaweza kuwa mazuri sana , kwamba mkutano huu wa kundi la mataifa ya G8 uliofanyika mjini Heiligendamm unaweza kukumbukwa katika historia kuwa alama ya dunia sio tu kwa mapambano dhidi ya ongezeko la ujoto duniani, lakini pia umoja baina ya mataifa tajiri na yale masikini.

Na pia mataifa hayo manane tajiri duniani yametambua kuwa , pekee hayawezi kutatua matatizo ya dunia , lakini yamesisitiza kuwa yanahitaji msaada kutoka China, India, Brazil , Mexico na Afrika kusini.

Pia mataifa hayo ya G8 hayataki kupanua kundi lao hilo, lakini watatayarisha mfumo mbao wataweza kufanya na mataifa hayo majadiliano, kama Angela Merkel katika mkutano huu wa Heilingendamm alivyoonyesha. Mataifa haya lakini hayawezi kuwamo ndani ya utaratibu huu. Mataifa masikini yanabaki katika meza ya majadiliano ya mkutano wa biashara.

Maandamano ambayo kila mara yanafanyika katika mikutano ya kimataifa , hayakuweza kuchafua majadiliano ya viongozi.

Ghasia hazikufanywa dhidi ya polisi tu , lakini pia kulifanyika maandamano ya amani. Mbinyo kutoka katika asasi zisizo za kiserikali umesaidia kuweza kupatikana msimamo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo ya amani na uhakika wa kuwa na amani. Mandamano yao yamewakutanisha vijana kutoka mataifa kadha na yamekuwa na maana kisiasa, yaliyotarajiwa.