1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Commonwealth umemalizika mjini Kampala

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSxR

Kampala:

Mkutano wa kilele wa viongozi wa taifa na serikali wa jumuia ya madola Comonwealth,ulioanza ijumaa iliyopita umemalizika hivi punde katika mji mkuu wa Uganda Kampala baada ya mijadala kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na kanuni za biashara ya kimataifa.”Mkutano wa kilele umemalizika” amesema rais Yoweri Museveni wa Ugada katika sherehe za kuufunga mkutano huo,zilizofanyika katika hoteli moja mashuhuri nje ya mji mkuu wa Uganda Kampala.Taarifa ya pamoja iliyotangazwa leo na kuvifikia vyombo vya habari,inakumbusha maadili ya kimsingi ya jumuia ya Commonwealth na kugusia masuala kuhusu kwa mfano upunguzaji wa silaha,ugaidi,haki za binaadam,biashara na ukimwi.Viongozi wameshindwa hapo jana kuafikiana juu ya msimamo wa pamoja dhidi ya kuchafuliwa hali ya hewa na namna ya kupunguza moshi wa viwandani.Jana viongozi wa jumuia ya madola Commonwealth walimchagua balozi wa India nchini Uengereza Kamalesh Sharma kua katibu mkiuu mpya.Atakabidhiwa wadhifa huo April mwakani , Don McKinnon wa kutoka New-Zealand atakapomaliza mihula miwili ya wadghifa huo wa miaka minne.Mkutano wa mwaka huu wa jumuia ya madola Commonwealth uligubikwa na kusitishiwa uanachama Pakistan na baraza la mawaziri.Hi ni mara ya pili kwa Pakistan kusimamishiwa uanachama baada ya kuachwa nje ,kwa muda wa miaka mitano baada ya mapinduzi yaliyomleta madarakani Pervez Musharaf mnamo mwaka 1999.