1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika

25 Julai 2010

Viongozi wa Umoja wa Afrika wanakutana katika mji mkuu wa Uganda Kampala.

https://p.dw.com/p/OUAp
(FILE) A file photograph showing Malawi's President elect Bingu wa Mutharika of the ruling United Democratic Front (UDF) speaking to the media on 20 May 2004 after casting his vote in the third Malawian democratic elections. It has been reported on 22 May 2009 that Malawi's President Bingu wa Mutharika has won a second five-year term in office, according to the country's electoral commission. The commission said that he had won 2.7 million votes, with his nearest rival John Tembo winning 1.2 million. EPA/STR +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi.Picha: picture-alliance/ dpa

Mada kuu itakayojadiliwa na viongozi wa Umoja wa Afrika katika mkutano wao inahusika na Somalia, hasa kufuatia mashambulio yaliyoua watu 76 mjini Kampala. Inasemekana kuwa mashambulio hayo yalifanywa na wanamgambo wa Kisomali Al- Shebab. Viongozi hao walibakia kimya kwa dakika mbili kuwakumbuka wahanga wa shambulio hilo la Julai 11.

Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi nchi inayoshika wadhifa wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amewalaani vikali wahusika wa shambulio hilo.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir hakuhudhuria mkutano huo wa kilele. Mapema mwezi huu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu iliongezea mashtaka ya mauaji ya kimbari dhidi ya Rais Bashir, kwa hivyo Uganda iliyo mwanachama wa mahakama hiyo, ingepaswa kumkamata kiongozi huyo wa Sudan.

Mwandishi:P.Martin/AFPE

Mhariri: M.Dahman