1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya Brussels

11 Desemba 2009

Vipi kuafikiana mchango wa Euro bilioni 6 ?

https://p.dw.com/p/KztR
Angela Merkel na viongozi wa Ulaya.Picha: DPA

Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika jaribio lao la kuhimiza zaidi maafikiano ya nchi zote ulimwenguni juu ya kupiga vita uchafuzi wa hali ya hewa huko Copenhagen,walivutana usiku mzima hapo jana huko Brussls, hadi kuafikiana leo mchango wao wa Euro bilioni 6 katika mfuko wa kuzisaidia nchi masikini zinazo athirika na janga hilo.

Wakati nchi 194 zinakutana mjini Copenhagen, zikijaribu kuapatana jinsi ya kuzuwia uchafuzi zaidi wa hali ya hewa kutokana na moshi unaopaa hewani, swali nani atabeba mzigo wa gharama zake , limebakia kuwa pingamizi katika njia ya kufikia mapatano yatakayo chukua nafasi ya itifaki ya Kyoto.

Nchi za Umoja wa Ulaya,zilikwisha pendekeza kwamba, Euro bilioni 100 zitolewe kuzisaidia nchi masikini kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2020 ili zipambane na kuzidi kupanda kwa kima cha maji ya bahari karika fukwe zao, katika kupambana na misitu yao kugeuka jangwa na kuzuwia kuenea kwa majangwa pamoja na matatizo mengine yanayohusiana nayo.

Lakini, baada ya siku ya kwanza ya kikao hapo jana, huko Brussels, viongozi wa Umoja wa Ulaya, walikuwa bado hawakukifikia kima hicho cha Euro bilioni 6 walicholenga.Juu ya hivyo, viongozi wa Umoja wa Ulaya ,wana yakini watatoa fedha hizo leo siku yao ya pili ya mkutano.

Leo waziri mkuu Gordon Brown wa Uingereza na rais Nicolas Zarkozy wa Ufaransa, walikuwa na mkutano na waandishi habari ambamo kwa pamoja walitangaza mchango wa nchi zao katika mfuko huo..

"Ulaya itatoa sehemu yake katika mfuko wa dala bilioni 10.Pia Ulaya itajitolea kutoa mchango wake katika ule mfuko wa dala bilioni 100 kila mwaka kwa gharama za muda mrefu tena kila mwaka hadi ifikapo 2020."-alisema Gordon Brown.

Usiku mzima jana, viongozi hao wa Umoja wa Ulaya, walijadiliana jinsi ya kuchangia Euro bilioni 2 kwa mwaka katika kile kilichopewa jina ,"mfuko wa kwanza wa fedha " kati ya mwaka ujao 2010-2012.

Kutokana na ahadi za nchi nyingi za UU ,miongoni mwa hizo,Sweden,Ubelgiji na Finland,tayari kabla kikao cha jana kuanza zilipatikana Euro bilioni 2. Hata Ujerumani itatoa mchango wsake kwa muujibu alivyosisitiza Kanzela Angela Merkel:

"Ujerumani , itachangia tangu kwa kipindi kifupi hata kirefu kijacho, katika kuzisaidia nchi masikini za dunia hii ili zijiwinde kwa mapambano ya mabadiliko ya hali ya hewa. Kwani, nionavyo mimi , hapo ndipo mafanikio ya mkutano wa Copenhagen yanategemea mno."

Hapo kabla,Ujerumani na Ufaransa zikijizuwia kutaja kima cha mchango wao katika mfuko huo.Mjadala huu moto moto kati ya nchi masikini na tajiri kuhusu nani ajitwike mzigo mkubwa wa gharama za kupambana na moshi unaochafua mazingira umepaliliwa moto na kuvuja habari ya mapatano yaliokwisha tungwa kwa manufaa zaidi ya mataifa ya kiviwanda.

Mwandishi: Henn,Susanne/ DW Brussels/

Ramadhan Ali/ AFPE

Mhariri:Abdul-Rah