1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kimataifa wa Annapolis

Oummilkheir28 Novemba 2007

Kufufuliwa upya utaratibu wa amani ya Mashariki ya kati baada yya Annapolis

https://p.dw.com/p/CU4j
Viongozi wa Israel na Palasatina wapeana mikonoPicha: AP

Ajenda ya mkutano wa kimataifa wa mashariki ya kati,ilikua ndefu.Mbali na hotuba kadhaa ,pembezoni mwa mkutano huo ,masuala kuhusu utaratibu wa amani na uungaji mkono wa kimataifa yalijadiliwa.Yamazungumziwa pia masuala kuhusu namna ya kutia njiani taasisi imara za utawala kwa wapalastina,uhusiano wa Israel na majirani zake na kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati yao.Hakujakua na matokeo mengi thabiti.Mkutano wa Annapolis ni mwanzo tuu wa utaratibu mzima wa amani na hilo limefanikiwa.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice ana matumaini mema baada ya kumalizika mkutano huo wa siku moja.Hii leo kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert wanatazamiwa kuanzisha rasmi mazungumzo ya pande mbili katika ikulu ya Marekani,mazungumzo yatakayomalizika kwa kuundwa madola mawili huru.Duru ya kwanza ya mazungumzo ya mazungumzo itafanyika December 12 ijayo.Muda mfupi baadae utaitishwa mkutano wa wafadhili mjini Paris na kufuatiwa na ule wa wawakilishi wa pande nne zinazosimamamia utaratibu mpya wa amani ya mashariki ya kati unaojulikana kama Roadmap.

Utaratibu huo ulioanzishwa September mwaka 2002,nao pia umefufuliwa.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice anasema:

“Pande zimekubaliana pia kutia njiani moja kwa moja utaratibu wa amani wa Roadmap,na kurahisisha masharti na kufungua njia ya kupatikana ufumbuzi wa madola mawili.Katika majadiliano yao pande hizi mbili zijadili kwa undani kabisa masuala yote yaliyoko,ikiwa ni pamoja na suala la kurejea wakaimbizi wa kipalastina,usalama,maji,maeneo ya wahamiaji wa kiyahudi na kanuni za Jerusalem.Haya ni makubaliano ya maana sana kwasababu katika kipindi cha miaka sabaa iliyopita,hakujawahi kufanyika majadiliano kama haya.”

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ameshadidia umuhim u wa kushiriki zaidi ya mataida 40 na mashirika katika mkutano huo.Amesifu hotuba ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa saud Arabia ambae ndie mwenyekiti wa sasa wa jumuia ya nchi za kiarabu.

Wajumbe wa Syria na Libnan pia walihutubia.

Balozi wa Saud Arabia nchini Marekani Adel al Jubeir amesema mazungumzo ya Annapolis ni hatua ya mwanzo muhimu katika utaratibu wa amani ya mashariki ya kati.

Hata muakilishi wa chama cha ukombozi wa Palastina PLo nchini Marekani Afif Safieh amesifu mazungumzo ya Annapolis akisema yanatia moyo.Amekiri hata hivyo,kuna walakini unaotokana na mfarakano ulioko miongoni mwa wapalastina na msimamo wa Hamas dhidi ya mkutano huo wa amani ya mashariki ya kati.

Hamas wanadai Mahmoud Abbas hana haki ya kuzungumza kwa niaba ya wapalastina.

Wawakilishi wa Hamas hawakualikwa kabisa katika mkutano wa Annapolis,rais Bush anasema wamejiharibia wenyewe.Lakini sio Hamas tuu wanaopinga mkutano huo,nchini Israel pia kuna wapinzani.

Makundi ya nadharia kali za mrengo wa kulia nay ale ya itikadi kali za kidini yamepaza sauti kulaani mkutano wa Annapolis.Chama cha Shas kimetishia kujitoa katika serikali ya muungano ya waziri mkuu Ehud Olmert.Hata chama cha nadharia kali za mrengo wa kulia kilichoundwa na wahamiaji wa kiyahudi kutoka Urusi ,Israel Beiteinu kinakosoa matokeo ya Annapolis.Kinasema kattu suala la Jerusalem halitojadiliwa.