1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa viongozi wa Kiangalikana duniani waendelea Daresalaam

14 Februari 2007

Viongozi wa kanisa la kianglikan duniani wamekutana katika jiji la Daresalaam Tanzania kujadili juu ya mustakabali wa kanisa hilo.

https://p.dw.com/p/CHK9

Hii inakuja wakati kanisa hilo linakabiliwa na kitisho juu ya kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja na kuruhusu maaskofu wanaofanya mapenzi ya aina hiyo

Kiasi cha viongozi 38 wa kanisa hilo wamekutana katika hoteli moja kilomita 30 kaskazini mwa jijini la Daresalaam nchini Tanzania.

Mkutano huo wa wiki moja unajadili mustakabali wa baadae wa kanisa la Kiangilikani hasa kuhusiana na suala la kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja na vile vile kuruhusu watu hao yaani mashoga na masenge kuwa maaskofu ndani ya kanisa hilo.

Askofu mkuu wa diyosisi ya eneo la kati mwa Tanganyika Donald Ntentemera amewaambia waandishi wa habari kwamba mkutano huo ni wa faragha na unalenga kuyatatua masuala yote nyeti yanayolihusu kanisa hilo

Mkutano huo unaoogozwa na Askofu mkuu wa Canterburry Rowan Williams unatarajiwa kuzusha tofauti kati ya viongozi wa kanisa hilo wan chi zinazoendelea kutoka Asia Afrika na Amerika ya kusini pamoja na wale wanaotoka katika nchi za magharibi.

Mwandishi wetu Badra Masoud amenifahamisha kwamba mkutano huo unafanyika huku kukiwa na ulinzi mkali na vile vile katika hali iliyogubikwa na usiri mwingi na hata waandishi wa habari hawakupewa ruhusa ya kuhudhuria.Ingawa katibu mkuu wa kanisa la Angikan nchini Tanzania DKT Mwita Akiri anasema hakuna usiri kwenye mkutano huo.

Katika nchi zinazoendelea ambako kanisa hilo linazidi kupanua mbawa uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja unapingwa vikali kwani viongizi wa kidini wa kanisa hilo wanasema ni dhambi kwa muumba lakini kwa upande wa nchi tajiri zilizoendelea viongozi hao wanasema kwamba kanisa lishughulikie zaidi masuala ya umasiki katika ulimwengu wa tatu,Ukimwi na kupungua kwa idadi ya waumini wa kanisa hilo la Angikani duniani.

Katika mkutano huo wa Daresaalam mashoga pamoja na wasagaji pia wamefika kutoa kilio chao kwa Askofu mkuu wa kanisa la Anglikan Rowan Williams.

Mashoga hao wanadai wataka kutambuliwa na kanisa hilo kikamilifu kama waumini wengine na kupewa haki zote kama ilivyo kwa wengine.

David Machklian ni shoga na ni mkurugenzi wa kundi la kutetea mashoga kutoka Nigeria

"Kinachonivutia kwa mwanamme mwenzangu ni hisia ambazo nimepewa na muumba wangu kwa sababu mimi sijaumbwa na shetani nimeumbwa na huyuhuyu mungu na mimi ni mkristo kamili ni mwana wa mungu vilevile.''

Kumekuwepo na hali ya mvutano katika kanisa hilo tangu kutawazwa kwa mhubiri Gene Robinson ambaye ni msenge na kanisa la Episcopol la Marekani kuwa Askofu wa New Hampshire mwaka 2003, Ni kutokana na hilo ndipo nchi zinazoendelea zilipokataa ufadhili kutoka kwa kundi la kanisa hilo ambalo linaunga mkono hatua hiyo na hali hiyo imesababisha kile kinachoonekana kama mvutano.